Papic: Kocha (Minziro) aliyekuwa na Yanga kambini anajua vizuri zaidi, amekuwa na wachezaji kwa siku zote kwa hiyo alijua alichokifanya. Mimi sikuwa na kibali cha kufanya kazi. Hilo nadhani kocha aliyekuwapo anajua zaidi. Mwanaspoti: Unadhani nani alikuwa mchezaji bora wa mechi? Papic: Hilo halina ubishi Okwi. Amesababisha mabao yote matano. Mwanaspoti: Unadhani anaweza kucheza Afrika Kusini au Ulaya? Papic: Aende Ulaya, soka lake ni kubwa, tatizo jingine ni kuwa akienda Afrika Kusini ni ngumu kwenda Ulaya, ila akienda Ulaya anaweza kuanza na timu ndogo baadaye akapata timu kubwa. Mwanaspoti: Vipi mwamuzi wa mchezo? Papic: Alichezesha vizuri sana. Yanga imefungwa mabao matano, lakini hakuna sehemu unaweza kumlaumu mwamuzi. Alifanya kazi nzuri. Mwanaspoti: Ungekuwa benchi la Yanga ungeweza kubadilisha matokeo? Papic: Swali zuri, lakini siwezi kukujibu. Mkataba wangu umekwisha na Yanga. Ila kila kitu kingekuwa kizuri kama wachezaji wangekuwa wanalipwa mishahara yao na kocha angekuwa analipwa na kutafutiwa kibali cha kazi. Mwanaspoti: Unashauri Yanga wafanye usajili wa nafasi zipi? Papic: Siwezi kutoa ushauri, sasa nafikiria kujiunga na timu nyingine. Lakini Yanga ina matatizo mengi. Mwanaspoti: Unajiunga na timu gani? Papic: Siwezi kusema hapa, pengine unajua. |
Tuesday, May 8, 2012
PAPIC AMPELEKA OKWI ULAYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment